Mgonjwa anywa lita 100 za maji kwa saa mbili

23Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mgonjwa anywa lita 100 za maji kwa saa mbili

Mkazi wa kijiji cha Maguu wilayani  Mbinga mkoani Ruvuma Erick Msuha  ayesumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayomsababishia kunywa  lita mia moja za maji kwa saa mbili ili aendelee kuishi anaomba msaada aweze kutibiwa.

Erick Msuha.

Mgonjwa huyo anasema matatizo yake  yamemuanza baada ya kupigwa na radi mwaka 1993 lakini katika miaka ya hivi karibuni hali imekuwa mbaya zaidi ambapo amekuwa akitumia lita 100 za maji ambayo huyatoa kwa njia kutapika na njia ya haja ndogo huku akicheua.

Baba wa mgonjwa huyo Bw. January Msuha anasema mwanae anateseka sana na hawezi kulala kutokana na yanayomsibu na wao wameuza kila walichonacho kumsaidia bila mafanikio na hivyo wanawaomba wasamaria wema kuwasaidia.

Chanzo: ITV

 

Habari Kubwa