Mgonjwa wa kwanza Virusi vya Corona nchini aomba msamaha

18Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe
Mgonjwa wa kwanza Virusi vya Corona nchini aomba msamaha

Mtanzania wa kwanza aliyethibitika kuwa na virusi vya Corona, Isabella Mwampamba mwenye umri wa miaka 46, amezungumza leo kwa njia ya simu na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuzua taharuki na kuwataka watanzania wasiwe na hofu bali wazidi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.

Isabella Mwampamba.

Akizungumza kwa njia ya simu moja kwa moja (Mubashara) wakati wa mkutano wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu uliofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kutoa taarifa juu ya maambuzi mapya ya corona na hali ya Isabela.

"Ninawaomba msamaha kwa kuwa mtu wa kwanza wa Corona hapa Tanzania na kutengeneza taharuki nchi nzima, hali yangu inaendelea vizuri maana siumwi chochote na nimekuwa nikipima homa kila siku kila siku,"amesema Isabella.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema mtandao wa watu 26 walioshirikiana na mgonjwa huyo wako chini ya uangalizi na vipimo vya sampuli vimeshapelekwa jijini Dar Es Salaam na majibu yatatolewa wakati wowote kuanzia sasa.

 

Habari Kubwa