Miili ya askari 3 waliokufa katika msafara wa rais Singida, waangwa

08Feb 2016
Singida
Nipashe
Miili ya askari 3 waliokufa katika msafara wa rais Singida, waangwa

Mkuu wa mkoa wa Singida ameongoza maelfu ya wakazi wa mkoa wa Singida pamoja na askari wa jeshi la polisi kwenye kuaga miili mitatu ya maafisa wa jeshi la polisi waliokufa kwenye ajali wakati wakisindikiza msafara wa rais.

Akitoa salamu kwa niaba ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshiwa Dkt John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Singida dakari Parseko Kone amesema rais amepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na amewatakia familia za marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Akieleza ajali ilivyo tokea kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Thobiasi Sedoyeka amesema gari lilikuwa likiongoza msafara wa rais lilipasuka gurudumu lambele upande wa kulia na dereva sajent Gerald Ntondo kushindwa kuli mudu, huku akitoa salamu kwa niaba ya makamda wa polisi Tanzania,

kamanda wa polisi mkoa wa Manayara ACP Kamilius Wambura.

Kwa upande wao viongozi wa madhehebu ya dini ya kikristo na kiislamu wamewata waumini kujiandaa mapema kwa sababu hawajui siku wa saa ambayo bwana atawa kuja chukuwa.

Akitoa wasifu wa marehemu hao mnadhimu mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Simon Haule amesema jeshi la polisi mkoani Singida limepoteza askari ambao walikuwa wana tegemewa katika utendaji wao wa kazi na miili hiyo ina safirishwa kwenda kwa maziko Miraji Mwegoro mkoa wa Dar-es-Salaam, Eliasi Mrope mkoa wa Mtwara na Geradi Ntondo mkoa wa Kigoma.

Habari Kubwa