Miili hiyo itaagwa kwenye ibada ya mazishi kuanzia saa 8 mchana katika Kanisa la Mtakatifu Marco wilayani humo.
Akizungumza na Chombo kimoja cha habari leo Julai 4, 2022 Mwenyekiti wa Kijiji cha Manzase, Charles Kangwe amesema mazishi hayo yatafanyika katika makaburi ya kila familia kuanzia saa 10 alasiri.
“Kila familia itazika katika makaburi ya familia lakini kuagwa wataagwa kwa pamoja katika Kanisa la Mtakatifu Marco hapa hapa Manzase” amesema Mwenyekiti huyo.