Milton Makongoro Mahanga afariki Dunia

23Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Milton Makongoro Mahanga afariki Dunia

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Ilala Milton Makongoro Mahanga, amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Milton Makongoro Mahanga.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama wa CHADEMA, Tumaini Makene, amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

"Ni kweli aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Ilala na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama amefariki asubuhi ya leo, alikuwa amelazwa tangu juzi Muhimbili, taarifa za kina zaidi tutazitoa baadaye" amesema Makene.

Milton Makongoro Mahanga, aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Habari Kubwa