Mimba zakatisha masomo wasichana 48

11Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mimba zakatisha masomo wasichana 48

WASICHANA 48 katika shule za msingi na sekondari wilayani Karagwe mkoani Kagera, wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo mimba.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata Peter, alisema wanafunzi 25 walipata mimba, wanne waliolewa na tisa walitoroshwa na kuacha masomo kwa mwaka 2016.

Adeodata alibainisha kwamba halmashauri hiyo imewachukulia hatua mbalimbali za kusheria wanaume wote waliohusika kuwapa mimba wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa Adeodata, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kufungua mashtaka na mpaka sasa baadhi yao wameshtakiwa na kuhukumimwa.

Hata hivyo, Adeodata hakufanya zaidi kuhusu adhabu za zilizotolewa na mahakama ukiwamo muda wa vifungo.

Hata hivyo, aliongeza kuwa zipo hatua kadhaa zinazoendelea kuchukuliwa katika halmashauri za kukabiliana na matukio hayo.

Miongoni hatua hizo, Adeodata alisema kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe inaimarisha idara ya jinsia na watoto na kuwezesha wasichana kutekeleza majukumu yao kwa jamii.

Habari Kubwa