MISA Tan yalaani mwandishi wa Mwananchi kupigwa na askari SMZ

21Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
MISA Tan yalaani mwandishi wa Mwananchi kupigwa na askari SMZ

MISA Tan inalaani vikali kitendo cha kilichofanywa na askari wa SMZ kumtesa,kumdhalilisha kumjeruhi na kumwaribia vifaa vya kazi na binafsi mwanahabari aliyekuwa kazini kama ambavyo wao walikuwa kazini.

Mwandishi wa habari alikuwa akitumiza wajibu wake wa kupiga picha ili kuhabarisha umma juu ya kilichokuwa kinaendelea dhidi ya Machinga,hakukua na sababu yoyote ya kumshambulia kama mwizi au mhalifu wakati aliwaonyesha kitambulisho cha kazi na kujieleza alichokuwa anakifanya.

Ikumbuke kuwa waandishi wa habari wanatekeleza wajibu wao kisheria,na katika utekelezaji wa majukumu yake tunaamini hakuvunja sheria yoyote,na kama alivunja sheria utaratibu wa kisheria ungechukuliwa dhidi yake na siyo kumuhukumu kwa kipigo na kuharibu vifaa vyake.

Tunaamini SMZ itachukua hatua madhubuti dhidi ya askari waliotenda kosa hilo linalominya uhuru wa upatikanaji taarifa kwa mujibu wa sheria ya Access to Information Act 2016, na uhuru wa kujieleza.

Tukio hili linatokea ikiwa Mei 3,mwaka huu,Tanzania itaungana na dunia kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari.Tunavisihi vyombo vya ulinzi na usalama kutambua ushirikiano baina yao na waandishi wa habari na siyo kujenga uadui kwa kuwa wote tunajenga nyumba moja (Tanzani)hakuna sababu ya kugombea fito.

Imetolewa na Salome Kitomari-Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania( MISA-TAN)

Habari Kubwa