Mizengo Pinda ataka utunzaji wa mazingira

15May 2021
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Mizengo Pinda ataka utunzaji wa mazingira

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amewataka wakazi wa Kata ya Zuzu wakiwemo wanafunzi wa shule ya Sekondari Zinje kuitunza miti 10,000 iliotolewa kwa udhamini wa Benk ya Exim ili kuifanya Dodoma kuwa kijani.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akijiandaa kupanda mti katika shule ya sekondari Zinje iliopo kata ya Zuzu.

Mstaafu Pinda amesema miti ni muhimu kwa jamii, hivyo Benk ya Exim imefanya jambo kubwa kwa kuleta miti hiyo ambayo itasaidia kuzuia mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema wanachi wa eneo hilo wanapaswa Kutoa ushirikiano wa kuimwagilia ili ikuwe vizuri.                                   

Naye Mkuu wa masoko wa Benk ya Exim, Stanley Kafu amesema wao kama Exim watahakikisha wanashirikiana na wakazi wa Kata ya Zuzu ikiwemo Shule ya Sekondari Zinje kuhakikisha miti hiyo inakuwa vizuri.                                

Amesema suala la maji watahakikisha wanashirikiana pamoja na serikali kuhakikisha yanapatikana.

Mkuu wa masoko wa Benki ya Exim, Stanley Kafu akiwa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo na wanafunzi wa Zinje Sekondari, akimwagilia mti alioupanda.

Habari Kubwa