Mke, mume mbaroni tuhuma za mauaji

24Jan 2022
Rose Jacob
MWANZA
Nipashe
Mke, mume mbaroni tuhuma za mauaji

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano wakiwemo mke na mume kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya watu watatu wa familia moja katika mtaa wa Mecco mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mwanza, Ramadhani Ng'anzi.

Tukio hilo lilitokea Januari 18 mwaka huu majira ya saa 5: 30 usiku, katika mtaa Mecco kusini wilayani Ilemela mkoani Mwanza, baada ya watuhumiwa Deoglas Vicent mwenye umri wa miaka 26 na mkewe Hajira Thomas (24) kupanga njama ya mauaji hayo.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mwanza, Ramadhani Ng'anzi, amewataja waliouawa kuwa ni mfanyabiashara, Mary Charles (42), mtoto wake, Jenifa Fredy (22) na msaidizi wa kazi za ndani, Monica Jonas (19) a,mbao walikatwa na panga sehemu mbali mbali za miili yao.

"Chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kibiashara kati ya marehemu Mary ambaye alikuwa akileta biashara zake kutoka Kigoma, kuwapatia baadhi ya watuhumiwa ambao walishindwa kumlipa fedha zake kisha kupanga njama ya mauaji hayo," amesema Ng'anzi.

Kamanda Ng'anzi amewataja watuhumiwa waliowakamata kwa kutekeleza mauaji hayo ni Thomas Jilala (26) msukuma mkokoteni, Hajira Thomas (23) fundi cherehani, Deoglas Vicent (31) muuza duka la vifaa vya umeme, Emmanuel Mathew (19) wanne hawa wote ni wakazi wa Buhongwa na Emmanuel Charles (36) kazi yake ni opareta wa mitambo katika mgodi wa Mwadui na mkazi wa Mecco kusini.

Habari Kubwa