Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kikaangoni

02Jun 2020
Na Mwandishi Wetu
SUMBAWANGA
Nipashe
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kikaangoni

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua kwa kutokusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.

Akiongea na viongozi wa Mkoa wa Rukwa kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani  Rukwa amesema haingii akilini kuona Halmashauri inakuwa na upotevu mkubwa wa mapato lakini hakuna hatua zozote zinazochuliwa dhidi ya watumishi wanaoshiriki upotevu huo. 

Amesema kuwa sababu kubwa inayosababisha Halmashauri nyingi kutokukusanya mapato kikamilifi ni kutokana baadhi ya viongozi kutokuwa makini katika kusimamia na kufuatilia kwa karibu ukusanyaji wa mapato  kwa baadhi ya watumishi ambao si waadilifu.

Jafo amefafanua kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa halmashauri ambayo imekuwa na upotevu mkubwa wa makusanyo ya mapato jambo ambalo huzorotesha  maendeleo kwa jamii.

“Mkurugenzi anawajibu wa kusimamia kikamilifu suala la ukusanyaji wa  mapato katika Halmashauri yake, inasikitisha kuona bado baadhi ya watumishi ambao si waaminifu wanakusanya fedha na kuziweka mifukoni na mkurugenzi hachukui hatua za kinidhamu, hii ni kinyume na utaratibu. amesisistiza Jafo  

Jafo amesema kuwa inasikitisha kuona baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo kutokuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato jambo ambalo fedha nyingi zinazokusanywa hazifiki katika Halmashauri husika na kusababisha kutofikia malengo waliojipangia katika Halmashauri Hisoka.

Wakati huo huo Jafo  amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha Hospitali 67 zilizojengwa na kukamilika zinaanza kutoa huduma kwa jamii  kuanzia Juni 8, 2020.

Amezitaka Hospitali hizo za Wilaya kuhakikisha zinaanza kutoa huduma kwa jamii kwa upande wa wagonjwa wa nje na mama na mtoto ili kuwapunguzia adha wananchi wanaotembea muda mrefu kutafuta huduma za afya nchini.

“Serikali imetumia gharama kubwa kujenga majengo mazuri nay a kuvutia lakini mengi bado hajaanza kutoa huduma, jambo hili halikubaliki kwani lengo la Serikali ni kutoa huduma bora za afya kwa jamii, naagiza Hospitali hizo zianze ktoa huduma haraka ili kuwasaidia wananchi wanaoteseka kufuata huduma hizo mbali na maeneo wanyoishi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Jafo yupo kwenye ziara ya siku moja kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa wa Rukwa ambapo ataweka jiwe la msingi katika Stendi ya Mabasi iliyoko Katumba Sumbawanga, maegesho ya  Malori Utengule na ufunguzi wa barabara zenye urefu wa km 11.577 kupitia mradi wa uboreshaji miji.

Habari Kubwa