Mmiliki kiwanda adai kuvamiwa na kuporwa

27Dec 2020
Samson Chacha
Tarime
Nipashe Jumapili
Mmiliki kiwanda adai kuvamiwa na kuporwa

MFANYABIASHARA wa nafaka na mmiliki wa kiwanda kidogo cha kubangua nafaka, Hezron Moronya, amedai kuvamiwa wakati akiingia nyumbani kwake usiku na kutekwa na kundi la watu wanane waliokuwa na silaha za moto.

Amedai wahalifu hao walifyatua risasi nne hewani kisha kumpora fedha alizokuwa nazo Sh. milioni 2.3, kitabu cha hundi na simu ya mkononi kisha kutokomea kuelekea Isebania, Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu tukio hilo, mfanyabiashara huyo:

"Mnamo Desemba 23 saa mbili usiku, nilifunga biashara yangu ya kiwandani kule Kijiji cha Sokoni hapa Sirari, nilichukua gari langu dogo kuelekea nyumbani kwangu karibu na kiwandani.

"Nilipofika nje ya lango la kuingia, nilipiga honi, familia ilifika kunifungulia lango la kuingia ndani...soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa