Museveni ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana jana na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield ambaye amesema Mataifa ya Afrika yako huru kununua nafaka kutoa Urusi lakini huenda yakachukuliwa hatua ikiwa yatafanya biashara katika bidhaa zilizowekewa vikwazo na Marekani kama vile mafuta ya Urusi.
Linda amefika Ikulu ya Uganda Jana na kuzungumza na Museveni, Mshirika wa Marekani ambaye bado hajalaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na ambaye ameonesha huruma kwa Urusi na hivi karibuni alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na kuahidi kuendelea kushirikiana nae.
Akiwa Uganda Linda amesema nchi za Afrika zinaweza kununua bidhaa za kilimo za Urusi, ikiwa ni pamoja na mbolea na ngano lakini akaongeza kuwa iwapo Taifa lolote la Afrika litaamua kushirikiana na Urusi mahali kulikowekwa vikwazo, basi litakuwa linakiuka vikwazo hivyo na itachukuliwa hatua na Marekani.