MOI yamtunuku cheti Dk. Magu kwa ubobezi wa tiba ya Nyonga

24Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
MOI yamtunuku cheti Dk. Magu kwa ubobezi wa tiba ya Nyonga

TAASISI ya Tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) imemtunuku cheti maalum Profesa Dkt. Narender Kumar Magu kwa ushiriki na utoaji mada za kibingwa katika matibabu ya Nyonga-

Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) Dkt. Samweli Swai (katikati) na Dk Edmund Ndalama (kushoto) wakimkabidhi cheti maalum Profesa Dkt. Narender Kumar Magu kwa ushiriki na utoaji mada za kibingwa katika matibabu ya Nyonga na matatizo ya mifupa aliyoyatoa katika mafunzo maalum yaliyoshirikishwa Madaktari takribani 100, Jijini Dar es Salaam.

na matatizo ya mifupa aliyoyatoa katika mafunzo maalum yaliyoshirikishwa Madaktari takribani 100, Jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na MOI yamefikia tamati leo Machi 23 ambapo bingwa huyo kutoka Nchini India ameweza kuwasilisha mada zaidi ya 10 juu ya matibabu ya nyonga.

awali akimkabidhi cheti cha shukrani na ushiriki mafunzo hayo ya siku mbili, Mkurugenzi wa Tiba wa MOI, Dkt. Samweli Swai kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, amemwelezea Dkt. Magu kuwa ni miongoni mwa watalaam bingwa wanaoheshimika Duniani hivyo kwa mafunzo aliyoyatoa yatasaidia kuongeza juhudi kwa Madaktari shiriki.

“Uongozi wa MOI umefarijika sana kwa uwepo Dkt. Magu. mlichokipata hapa ni uzoefu tosha na itachochea haswa vijana wanaosomea Udaktari kuibukia kwenye kada hii na kuwa wabobezi." alieleza Dkt . Swai.

Ambapo aliongeza kuwa, kwa sasa wanayo nafasi ya kuhakikisha wanakuwa watalaam zaidi na hata kupata msaada wa kuwasilisha maandiko yao ili yaweze kupitiwa na Dk Magu huku akitoa wasaha kwenda kujifunza kwa vitendo zaidi.

Naye Profesa Dkt.Magu ameshukuru taasisi ya MOI kwa kuandaa tukio hilo ambapo amewataka wawe na kitu hicho mara kwa mara na amewakaribisha Madaktari kumtembelea kwenye huduma zake Nchini India ili wajifunze zaidi kwa vitendo.

Katika mafunzo hayo, Profesa Dkt Magu aliweza kuwasilisha mada za kibingwa juu ya nyonga zaidi ya 10 ambapo pia aliweza kuonesha uzoefu wake namna ya kutibu na kufuatilia maendeleo ya wagonjwa wake kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Kwa upande wake Dkt. Kennedy Nchimbi kutoka taasisi hiyo ya MOI alieleza kuwa tatizo la nyonga Tanzania ni kubwa ambapo mbali na ajali pia tatizo hiko usababishwa na ukosefu wa lishe bora.

"Tatizo la nyonga linaweza kukupata mbali na ajali ni kutokuzingatia lishe bora. Tunashauri watu wawe na utaratibu wa kucheki afya na nyonga ukiiwahi mapema inatibika na sio mpaka ikusumbue ndio utafute tiba.

Lakini pia tiba hii ya nyonga ikiwemo kuwekewa nyonga bandia ni gharama hivyo tuwe makini na miili yetu " alieleza Dkt. Nchimbi wakati akizungumza na wanahabari muda mfupi wa kuhitimisha tukio hilo.

Madaktari bingwa na Wanafunzi wa Vyuo vikuu vya Udaktari wameshiriki mafunzo hayo.
Miongoni mwa washiriki ni pamoja na Madaktari kutoka Hospitali zote kubwa na za mikoa ikiwemo Bugando, Mbeya, KCMC, Kairuki, Dodoma, Arusha na zingine.

Habari Kubwa