Mongella amshukuru Rais Samia utekelezaji daraja la Magufuli, Busisi

19Apr 2021
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Mongella amshukuru Rais Samia utekelezaji daraja la Magufuli, Busisi

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa nguvu alizowekeza kwenye utekelezaji wa miradi hasa daraja la Magufuli ambalo daraja wezeshi limekamilika kwa asilimia 100 huku daraja la kudumu likifikia asilimia 26.

Akizungumza baada ya kuvuka daraja hilo kutoka Kigogo kwenda Busisi wakati wa ukaguzi wa miradi amesema eneo ilo nilakimkakati hivyo wanawekeza nguvu katika maeneo hayo kama lilivyo agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwani daraja hilo litakalogharimu billion 700 na lenye urefu wa mita 3200 na upana wa mita 28.45  ujenzi wake utakapokamilika litakuwa kiungo cha kukuza uchumi wa mkoa na Taifa.

Aidha amewapongeza wakandarasi, TANROADS na wafanyakazi wote kwani kasi ya kutekeleza mradi huo ni kubwa na unaendelea bila kukwama.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mkoa wa Mwanza, Vedastus Maribe, amesema baada ya daraja wezeshi kukamilika kwa sasa nguvu zao wamezielekeza kwenye daraja la kudumu huku matarajio yao kukamilisha kwa wakati au kabla ya wakati.

Amesema serikali imewekeza nguvu kubwa hapo hivyo watafanya kazi ipasavyo ili wananchi waweze kupata fursa kupita katika daraja hilo.

Habari Kubwa