Moto soko la Karume wateketeza asilimia 98 ya vibanda na mali

16Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Moto soko la Karume wateketeza asilimia 98 ya vibanda na mali

ASILIMIA 98 ya vibanda na mali zilizokuwemo katika soko la Karume jijini Dar es Salaam vimeteketea na moto uliowaka katika soko hilo usiku wa kuamkia leo Januari 16, 2022.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya Ilala, Alisa Mugisha, ambapo amesema taarifa za moto huo walizipata baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja .

"Na kwa bahati nzuri wakati huo tulikuwa tunatoka mabibo ambako nako kuna nyumba ilikuwa inaungua moto na tulifika hapa ndani ya muda mfupi tulifika eneo la tukio lakini moto ulikuwa mkali kutokana na asili ya bidhaa wanazouza hapa mbao, maturubahi na nguo na vinasambaza moto kwa haraka tulijitahidi kuzunguka soko na kuanza kuzima,"amesema

"Tunachoshukuru Mungu hakuna madhara kwa binadamu na wala moto haukuvuka kwenda kwenye nyumba za wananchi kwa sababu tulikuwa na gari nne moja kutoka Kinondoni,Ilala, Bandari na Airport," amesema

Habari Kubwa