Mradi wa maji Kisarawe kuchochea wawekezaji- DC Jokate

12Jul 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mradi wa maji Kisarawe kuchochea wawekezaji- DC Jokate

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ameishukuru Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa) kwa kupeleka mradi wa maji katika wilaya ya Kisarawe utakaosaidia kuchochea idadi ya wawekezaji na viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ziara iliyofanyanywa na Mwenyekiti wa bodi ya Dawasa, Jenerali Davis Mwamunyage, Mwegelo alisema kuwa lengo ni wakazi wa Kisarawe na vitongoji vyake wapate maji ili wawekezaji wajitokeze kwa wingi.

“Mradi huu utasaidia wakazi wa Kisarawe na viunga vyake kupata maji na tunatoa nafasi kwa wawekezaji waje kuwekeza kwa wingi kwa sabababu Kisarawe inaendelea kukua kwa kasi hasa kwa sababu tunapata maji ya uhakika,”alisema Mwegelo.

Mwegelo alisema wawekezaji katika wilaya hiyo wanakabiliwa na changamoto za kukosa maji na umeme na hivyo mradi huo utajkapokamilika utaongeza idadi ya wawekezaji wa sekta ya viwanda.

“Kuna changamoto nyingi sana katika wilaya hii kubwa sana ni maji na umeme, naamini mradi huu wa maji utakapokamlika utamaliza changamoto hizi, hivyo nawakaribisha wawekezaji waje kwa wingi kuwekeza,”alisema Mwegelo.

Mwegelo aliongezea kuwa maendeleo ya mradi huo ni mazuri na kwamba wanatarajia wakati wa mwenge wa uhuru utakapo tembelea katika wilaya hiyo wataenda kuutembelea.

Habari Kubwa