Msajili aionya Chadema kuongeza Beti nyimbo ya Taifa

04Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Msajili aionya Chadema kuongeza Beti nyimbo ya Taifa

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mstaafu Francis Mutungi, ametoa onyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutokana na alichokiita ni uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza Beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mstaafu Francis Mutungi.

Mstaafu Jaji Mutungi ametoa onyo hilo mara baada ya chama hicho kuongoza Beti katika nyimbo hiyo jana wakati  wa vikao vya kupitisha jina la atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais.

Jaji Mutungi amesema kuwa kitendo khicho kilichofanywa na Chadema hakutegemea kwani ni chama kikongwe.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa kwa mujibu wa katiba ni kosa, huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kukumbuka kwamba sheria hazijakwenda likizo.

 

Habari Kubwa