Msalaba Mwekundu wajipanga kumuaga Magufuli Dodoma

21Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Msalaba Mwekundu wajipanga kumuaga Magufuli Dodoma

WAKATI maandalizi ya kuupokea mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli yakiendelea Jijini Dodoma, Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limejipanga vizuri katika kukamilisha majukumu yake.

Dk. John Magufuli.

Mratibu wa shirika hilo mkoani Dodoma, Michael Mshingo, amesema wameweka mahema makubwa mawili uwanjani hapo kwa kushirikiana na vikosi vingine ili kuhakikisha utaratibu unakuwa mzuri.

“Tuna kikosi imara cha kutoa huduma, tumejipanga na vifaa vyote tunavyo tunaamini hakutakuwepo na upungufu wa namna yoyote katika shughuli hii, Watanzania watuamini,” amesema Mshingo.

Shughuli ya kuuwaga mwili utafanyika Kesho Machi 22, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri jijini humo.

Habari Kubwa