Msimamo Spika ripoti ya CAG

25Apr 2018
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Msimamo Spika ripoti ya CAG

SPIKA Job Ndugai amesema mawaziri hawafungwi mdomo kuzizungumzia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), lakini taratibu za Bunge katika kushughulikia hoja hizo zitaendelea kuzingatiwa.

Kiongozi huyo wa Bunge alitoa kauli hiyo bungeni mjini hapa jana alipojibu mwongozo ulioombwa kwake na Mwita Waitara.

Mbunge huyo wa Ukon- ga (Chadema) alihoji kwa Spika uhalali wa mawaziri hao kuendelea kujibu hoja zilizoibuliwa na CAG katika ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2016/17.

Katikakujengahojayake, Waitara alisema Waziri wa Nchi, O si ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ni miongoni mwa mawaziri waliokiuka taratibu za Bunge kwa kuwa juzi ali- zungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge na kujibu hoja za CAG zilioelekezwa wizarani kwake.

Alisema kitendo hicho pia ni mwendelezo wa vitendo hivyo kwa mawaziri wa seri- kali ya awamu ya tano kujibu hoja za CAG hadharani.

Waitara alieleza kuwa taratibu za Bunge zinataka taarifa ya CAG zikishatoka serikali itafute majibu na wahusika waende kutoa majibu hayo kwa kamati husika za Bunge (PAC na LAAC).

“Lakini, mjada- la unaoendelea juu ya fedha Sh. trilioni 1.5, maana yake ni kama wabunge tumechanganywa utaratibu upi tunatakiwa kufuata. Katika kujadili mambo haya ni kwenye taarifa au kila mmoja anasema ya kwake?” Alisema Waitara.

Mbunge huyo alisema kwa kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ipo na inafanya kazi kwa niaba ya Bungezima,basimchakato wa kuchunguza matumizi ya fedha hizo ufanywe na kamati hiyo kwa sababu kuna wengine wanasema fedha zimeibwa wengine wanasema fedha hazijaibwa.

“Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa hivyo naomba mwongozo kwa sababu wanaendelea kuso- ma taarifa hizo na jana ( juzi) Jenista alikuwa akizungumzia habari ya vyama na hasa Chadema kwamba kuna fedha zimeibiwa na humu vimetajwa vyama tisa na amezungumza Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkopo uliotolewa bila viambatan- isho,” alisema.

“Ili tusichanganye wananchi, tungepata mwongozo wako utaratibu wa kufuatwa, kauli ya serikali ni ipi? Wabunge waseme nini? Kama taifa tusimamie kitu gani? Mheshimiwa Spika naomba mwongozo wako katika jambo hili.”

Akimjibu mbunge huyo, Ndugai (pichani) alisema suala hilo liliishatolewa ufafanuzi na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, kwamba mawaziri hawafungwi mdomo kuizungumzia ripoti ya CAG. “Maelezo ni hayo hayo;

hatuwezi kufunga mdomo mawaziri kutoa maoni yao... hawajasema hapa (ndani ya Bunge) wamezungumza huko walikozungumza,” alisema Ndugai.

Spika huyo alisema ham- na shida na utaratibu wa kawaida unaendelea tu kwa mujibu wa kanuni za Bunge zilizopo.

“Mwenyekiti (wa PAC) yupo, hakuna tatizo na Bunge linaendelea na mchakato wake kama kawaida na anayeamua ku- zungumzia, azungumzie tu kama kawaida, hamna shida, kama Chadema imetajwa tumia, tumia basi nimemsikia hata mwakilishi wa Chadema naye akilizungumzia kwamba hawa- jala hela, kwa hiyo, wote wanaendelea tu, hakuna shida.”

Tangu Aprili 15, ikiwa ni siku moja baada ya CAG Prof. Mussa Assad, kuwasilisha bungeni ripoti yake ya ukaguzi ya mwaka 2016/17, mawaziri wamekuwa waki- zungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizoibu- liwa na CAG na kuelekezwa kwa wizara zao.

Hata hivyo, utaratibu huo mpya wa serikali umeping- wa vikali na wenyeviti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka na LAAC, Vedasto Ngambe Mwiru ambao wiki iliyopita waliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa unakiuka taratibu za Bunge na sheria iliyoanzisha O si ya Taifa ya Ukaguzi, ambayo CAG ni mkuu wake. 

Habari Kubwa