Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu akutwa amefariki

28Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu akutwa amefariki

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limethibitisha kutupwa kwa mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa ITV/Radio one na Mtayarishaji wa kipindi cha Jarida la Wanawake Blandina Sembu katika eneo la njia panda ya ITV na watu wasiojulikana.

Blandina Sembu.

Kamanda wa Polisi, Ramadhan Kingai, ameeleza kuwa wamepata taarifa za mwili wa Blandina kutupwa mbele ya baa ya Maryland majira ya saa tano usiku akiwa tayari amefariki.

Amesema gari aina ya Toyota Noah ilifika katika eneo hilo na kusimama kwa muda mfupi kabla ya kutupa mwili wa Blandina.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa bodaboda waliokuwa wamepaki jirani na eneo hilo walishuhudia gari lililowashaa taa likisimama kwa dakika mbili kisha wakaona mwanamke ametupwa.

“Uchunguzi unaendelea ila tulichobaini huyu mtu hakuuliwa pale, mauaji yalifanyika sehemu nyingine pale walienda kumtupa” amesema Kamanda Kingai.

Habari Kubwa