Mtanzania atwaa tuzo haki za binadamu

19Jan 2022
Faustine Feliciane
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mtanzania atwaa tuzo haki za binadamu

SERIKALI ya Ujerumani na Ufaransa jana imekabidhi tuzo ya Haki za Binadamu kwa Mtazania, Noellah Msuya kupitia Taasisi yake ya kusaidia watoto wasiojiweza na wenye uhitaji maalum ya 'Child Support Tazania' (CST).

Tuzo hiyo imetolewa baada ya Serikali hizo kutambua mchango wa Noellah, pamoja na taasisi yake kwa watoto zaidi ya 600 wanaowasaidia.

Akizugumza wakati wa kukabidhi tuzo hiyo kweye hafla iliyofayika nyumbani kwa Balozi wa Ujerumai nchini Tanzaia, Balozi Regine Hess alisema kuwa tuzo hiyo imetolewa na Serikali za nchi hizo kupitia kwa mawaziri wao wa mambo ya nje, Annalena Baerock na wa Ufarasa Jean-Yves Le Drian.

Alisema kila mwaka inapofika Desemba 10 siku ya Haki ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Ujerumani na Ufaransa zinatoa tuzo hiyo kuthamini mchango na juhudi za taasisi au mtu mmoja mmoja kweye kusaidia wengie kupata haki zao.

"Tuzo hii imetolewa kwa taasisi na watu binafsi 15 tu Duniai kote, na kwa bahati nzuri Tanzaia ni miongoni mwa nchi ambayo mtu au taasisi iliyopo nchini imepata tuzo hiyo, tuna mpongeza Noelah na tasisi yake kwa tuzo hii," alisema Balozi Regine Hess.

"Noelah na taasisi yake wanatoa haki za msingi kwa watoto wenye ulemavu,haki hizo ni pamoja na kupata elimu na mahitaji mengine," alisema Regie.

Balozi Regine amezitaja nchi nyingine zilizotoa washindi wa tuzo hiyo kuwa ni Afghanistan, China, Haiti, Ufilipino, Iran, Lebanon, Uturuki, Afrika Kusini, Nigeria, Venezuela, Benin, Myanmar, Bosnia na Tanzania.

Aidha, kwa upade wake Balozi wa Ufarasa nchini Tanzania, Nabil Hajlaoui alimpongeza Noelah na kumtaka kuedeleza juhudi zake za kusaidia watoto wasiojiweza na wenye uhitaji.

Aidha, akizugumza wakati akipokea tuzo hiyo, Noelah ambaye ni Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya CST inayojishughurisha kuwasomesha na kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa ania mbalimbali, alisema tuzo hiyo imempa moyo wa kuendelea kupambana kuwasaidia watoto wenye uhitaji.

"Wakati naanza sikutegemea kama mchango wangu utathaminika hivi, awashukuru wadau wote ninaoshirikiana nao ikiwemo Serikali ya Tanzania.

Alisema lego la taasisi yake ni kufikia mikoa mingi zaidi kuwasaidia watoto kwa kujenga shule za mfano kwa ajili ya watoto weye ulemavu.

Kwa sasa CST yenye Makao Makuu yake jijini Mbeya inahudumia shule za msingi 30 za mkoa huo pamoja na kutoa elimu kwa walimu jinsi ya kuhudumia watoto wenye ulemavu.

Habari Kubwa