Mtoto aliyezama baharini anatafutwa

08Nov 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mtoto aliyezama baharini anatafutwa
  • *Familia yaomba msaada kwa atakayemwona atoe taarifa

Awadhi Hassan Omary Matondo (pichani) mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mizimbini Kibada Kigamboni amepotea na hajulikani alipo baada ya kuzama baharini alipokuwa akiogelea na wenzake South Beach Kigamboni.

Awadhi Hassan Omary Matondo.

Siku ya Novemba 06 mwaka huu, huko South Beach Kigamboni, Awadhi na wenzake watano walikuwa wakiogelea kwa bahati mbaya walizama, mmoja wao alijiokoa mwenyewe, watatu waliokolewa lakini mmoja wapo alikuwa tayari amefariki dunia, wawili kati yao wanaendelea vizuri. 

Awadhi mpaka leo Novemba 08 mwaka huu bado hajapatikana wala mwili wake kuopolewa.

Tunaomba kwa yoyote atakaye uona mwili wake sehemu yoyote, apige simu kwenda namba hii ya Voda 0754318762 Au 0787332246 jina Omary Matondo. Asanteni kwa ushirikiano na Mungu atusaidie.

Habari Kubwa