Mtuka aishauri ATCL mambo manne kupata mapato mengi

17Jun 2019
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Mtuka aishauri ATCL mambo manne kupata mapato mengi

MBUNGE wa Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka ameshauri mambo manne ambayo kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), ili kupata mapato mengi.

Aidha amesema kuwa Shirika hilo haliwezi kuendeshwa kwa tiketi peke yake kwa kuwa si biashara ya ndege na kwamba endapo mambo hayo yakifanyika wasafiri watasafiri kwa bei ya sh. 100,000 tu kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Mtuka ametoa ushauri huo jijini hapa leo wakati akichangia kwenye hotuba ya Bajeti kuu ya serikali na Mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Mbunge wa Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka.

Amesema Serikali imenunua ndege kubwa sita na inaendelea lakini uuzaji tiketi peke yake haziwezi kuendesha shirika hilo na badala yake kuna shughuli nyingi ambazo zinaweza kufanywa ATCL ikawa na shirika tanzu yakawepo madogo madogo ya kuendesha shughuli hizo.

Ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na kuwepo shirika dogo ambalo linaendesha shughuli za kuhudumia mizigo ambazo zinafanywa na mashirika mengine ya ndege ili kufanya huduma hiyo kwa ndege za ATCL na kampuni nyingine kutengeneza fedha.

"Tutaokoa fedha kwenye kampuni yetu lakini pia tutafanya huduma kwenye ndege nyingine hivyo kutengeneza fedha,"amesema

Ametaja pia ifanyike shughuli ya vyakula na hoteli kwenye ndege kwa kuanzisha kampuni ndogo ya kuuza chakula kwenye ndege  na za nchi nyingine.

"Tatu, ianzishwe tozo ambazo ndege inapotua hawaelewi hali ya hewa kutokana na taa kuwachanganya zikiwemo malipo ya maegesho ambazo gharama yake inakadiriwa kuwa sh. Bilioni moja kwa mwezi ambapo ATCL inalipa,"amesema

Ameeleza  nchi nyingine kama Ethiopia Airlines, Emirates, Katar Airways, hayo ni mashirika ya serikali lakini hawalipi hizo tozo hivyo wanaokoa fedha nyingi  wakifanya hivyo kwa kiasi kikubwa.

Kadhalika, amesema kuwa kuna chuo cha ATC kinachofundisha wahudumu wa ndege ‘AIR HOSTS’ hakifundishi Marubani hivyo kushauri kianzishe kozi ya kufundishia marubani hao.

“Kwa mfano wanaenda kufundishiwa nchi nyingine lakini tukisema tuanzishe kosi za kuwafundisha maribani ili wafundihswe hapa nchini itakuwa nafuu maana kufundisha rubani mmoja mwaka mmoja nje ni sh. milioni zaidi ya 80 kikianzishwa hapa tutapunguza gharama,”amesema.

Mtuka amesema kuna baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege huwa wanakuwa na bidhaa ambazo zinahitaji kutunzwa hivyo ni vyema yangeanzishwa mahandaki 'GoDowns' ya kutunzia bidhaa hizo ili safari ikikaribia kuanza achukue kwa kulipia ambapo serikali itapata fedha nyingi.

“Nasisitiza kuwa tiketi peke yake si biashara ya shirika la ndege mambo hayo manne yakizingatiwa tutaenda hata kwa laki moja Dar es Salaam kwa kutumia ndege zetu kwakuwa tutakuwa na fedha nyingi hivyo nauri zitapungua,”amesema.

Habari Kubwa