Mufti aelekea Ujerumani

20Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mufti aelekea Ujerumani

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, anaondoka leo kuelekea Ujerumani kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ushirikiano katika imani unaokutanisha dini mbalimbali.

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir.

Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Horera Tabu, alisema Mufti anaondoka usiku kuelekea Ujerumani kuhudhuria mkutano huo wa siku nne.

Tabu alisema ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuandaa mkutano huo ambao unahusisha dini mbalimbali na kwamba watajifunza masuala ya imani.

Aidha, alisema Mufti Zubeiry alirejea juzi kutoka Morocco, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa taasisi ya Mfalme wa Morocco ijulikayo kama Mohammed V6 Foundations.

Alisema Mufti alikuwa mjumbe kwenye mkutano huo ambao ulifanyika kwa siku nne akiwakilisha nchi za Afrika Mashariki.

“Morocco yeye alikuwa mjumbe kwenye mkutano wa taasisi ya Mfalme Mohammed V6 na yeye Mufti alikuwa anawakilisha East Africa Kwenye mkutano huo,” alisema Tabu.

Habari Kubwa