Mufti apiga marufuku upigaji wa Qaswida kiholela

10Dec 2019
Kelvin Innocent
Dar es Salaam
Nipashe
Mufti apiga marufuku upigaji wa Qaswida kiholela

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir, amepiga marufuku muziki wa Dufu pamoja na Qaswida, (Muziki Moto) kwa nchi nzima kwa watumiaji wa dini ya Kiislamu.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir, picha mtandao

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kusema kwamba aina ya miziki hiyo huiaibisha dini hiyo na kuichafua pamoja na kuonekana siyo dini yenye maadili kama zilivyo dini zingine.

Hata hivyo Zubeir amewataka wanaofanya shughuli za miziki ya aina hiyo, kuacha kufanya hivyo mara moja.

“Ninawataka wanao fanya hivyo kwa jina la Uislamu kuacha mara moja Uislamu ni dini yenye maadili mema na mafunzo sahihi yanayotokana na kitabu kitakatifu ‘Quran',” amesema Zubeir.

Pia amsema ni vibaya kwa dini kutafsiriwa vibaya kwa makosa ya watu kadhaa hasa wanao jishughulisha na miziki hiyo, hivyo amewataka kuachana nao kwa sababu huchafua sura ya dini hiyo.

Habari Kubwa