Mume amtelekeza mke mgonjwa kwa mama mzazi

27Sep 2021
Richard Makore
MWANZA
Nipashe
Mume amtelekeza mke mgonjwa kwa mama mzazi
  • Mgonjwa aomba msaada wa matibabu...

VERONICA Chacha (27) mkazi wa Buswelu mtaa wa Isenga mkoani Mwanza amewaomba Watanzania wenye moyo na uwezo kumsaidia gharama za matibabu ya figo, uvimbe tumboni na vidonda vya tumbo ambavyo vimemsumbua kwa muda wa miaka nane sasa.

VERONICA Chacha.

Veronica, ambaye ni mama wa watoto wawili alianza kuugua mwaka 2013 sasa amepooza miguu huku mume wake akimtelekeza kwa mama yake mzazi bila matunzo na kwenda kuoa mke mwengine.

Akizungumza na Nipashe Digital leo Septemba 27,2021 iliyofika nyumbani kwa mama mkwe wake Veronica, mtaa wa Isenga, amesema alipata vipimo katika hospitali ya Rufani ya Kanda ya Bugando lakini ameshindwa kupata matibabu kutokana na familia yake kukosa uwezo wa kulipa gharama.

Amesema kutokana na hali hiyo alirudishwa nyumbani na kwamba anazidi kuteseka kwa zaidi ya miaka nane bila msaada wowote wa matibabu.

Kwa upande wake, dada wa mgonjwa huyo, Rosemary Chacha amesema mdogo wake, ameumwa kwa kipindi kirefu na kwamba familia haina uwezo wa kugharamia matibabu yake.

Mama mkwe wa Veronica, anayemuuguza nyumbani kwake  amesema, yeye hana uwezo wa kifedha na kuwaomba watanzania, wakiwamo wafanyabiashara na kampuni mbalimbali kujitokeza na kumsaidia kwa kuwa mgonjwa anapitia maumivu makali bila ya kupata matibabu.

KWA MSAADA WA MATIBABU WA VERONICA WASILIANA NA

JINA: ROSEMARY CHACHA

NAMBA: 0762-932019