Mvua ya upepo yasababisha maafa Bariadi

27Feb 2019
Happy Severine
BARIADI
Nipashe
Mvua ya upepo yasababisha maafa Bariadi

Upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana Wilayani Bariadi ,Mkoani Simiyu imesababisha uharibifu mkubwa wa nyumba 25,vyumba vya madarasa vinne  pamoja na kifo cha mtu mmoja  katika kijiji cha Mwauchumu Wilayani huko.

kamishina msaidizi wa polisi, Benjamini Kuzaga (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Mwauchumu Mara baada ya kukagua moja ya chumba cha madarasa kilichoharibiwa na mvua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hill, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP William Mkonda amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jana   april 24,mwaka huu katika kijiji cha Mwauchumu ambapo jumla ya nyumba 21, vyumba vya madarasa 4  vya shule ya msingi Mwauchumu viliharibika vibaya sana na kubomoka ,pamoja na kifo mtu mmoja aliyejulikana kwa Hindu Desi (105) mkazi wa kijiji hicho.

Aidha Kamanda Mkonda amesema mbali na kutokea kifo huyo pia kuna majeruhi wawili Nkamba Rugaka(65) na Nkama Charles (52) ambao wote  wanaendelea na matibabu katika zahanati ya Mwauchumu Wilayani humo.

Baadhi ya majengo ya shule na nyumba za wananchi zikiwa zimeharibiwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha Ester Ipilinga Mwauchumu amesema kuwa mvua hiyo imesababisha wananchi wake kukosa sehemu za kuishi na kwamba utaratibu wa kuwasaidia unaratibiwa na kitendo cha maafa huku akiwahakikishia wahanga hao kupatiwa msaada.

 

 

Habari Kubwa