Mvua ya siku tatu yaua tisa Dar

16Apr 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mvua ya siku tatu yaua tisa Dar

Watu tisa wameripotiwa kupoteza maisha huku sita wakijeruhiwa kwa kudondokewa na ukuta kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Aprili 16,2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, LazaroMambosasa amesema watu hao wamefariki kutokana na mvua za siku tatu mfululizo ambapo baadhi yao walikutwa wanaelea kwenye mito mbalimbali na wengine kuangukiwa na ukuta.

“Leo nimezunguka kwa helkopta kwa kweli maeneo mengi yameathirika kutokana na mvua zinazoendelea na kusababisha madaraja kuondoka na sehemu nyingine maji kupita juu ya barabara ikiwemo eneo la Kijichi, Buguruni, Jangwani na Kigamboni," amesema Mambosasa. 

Habari Kubwa