Mwafrika wa kwanza apona corona kwa kutumia ARV

17Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mwafrika wa kwanza apona corona kwa kutumia ARV

Mwanafunzi raia wa Cameron amesimulia jinsi dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi zilivyomponya corona (covid-19).

Aidha, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 aliyeambukizwa virusi hivyo nchini China alisema katika kipindi chote cha matibabu yake yaliyodumu kwa siku 13 alikuwa akipewa dawa za antibiotiki na ARV.

 Kem Senou Pavel Daryl anayeishi katika mji wa Guangzhou alisema alianza kupata homa kali, kukohoa vibaya na kuonyesha dalili za mafua na baada ya vipimo aligundulika kuambukizwa virusi vya corona.

Akisimulia mkasa huyo, mwanafunzi huyo alisema ingawa alikuwa katika maumivu makali hakuwa na mpango wa kuondoka China hata kama hilo lingewezekana.

“Niliwaza sana, chochote kitakachofanyika sitaki kupeleka ugonjwa Afrika,” alisema mwanafunzi huyo akiwa katika chumba eneo maalumu alilotengwa kwa siku 14 sasa.

Alisema alipokuwa akieenda hosipitali kwa mara ya kwanza aliona kifo lakini baada ya kupewa dawa za kutibu wagonjwa walio na virusi vya ukimwi na antibiotic kwa wiki mbili alianza kuonesha dalili ya kupona.

Pavel Daryl ni mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrika aliyepona baada ya kuambukizwa na virusi hatari vya corona ambako sasa umeingia barani Afrika.

Habari Kubwa