Majaliwa aweka jiwe la msingi bandari ya Karema

05Jul 2020
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Majaliwa aweka jiwe la msingi bandari ya Karema

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa bandari ya Karema iliyopo katika Kata ya Karema wilayani Tanganyika mkoani Katavi ambayo Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi Billion 47 kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo.

Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Kassim Majaliwa akikata utepe katika uwekaji wa jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa Bandari inayojengwa Karema Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi.

Majaliwa ameweka jiwe hilo Julai 4, 2020 kwa lengo la kuhamasisha bandari hiyo iweze kukamilika kwa haraka na kuanza kufanya kazi.

Majaliwa amesema kukamilika kwa bandari hiyo mkoani humo kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kutokana na biashara za usafirishaji wa mizigo na abilia  kutoka Tanzania kuelekea nchi jirani kama vile Congo, burundi na Zambia.

Majaliwa pia amezindua jengo la biashara liliojengwa na Shirika la Nyumba Tanzania ( NHC) nakupewa jina la Mpanda Plaza ambapo amesema jengo hilo limeleta taswira mpya ya mji wa Mpanda.

Hata hivyo amelipongeza shirika hilo kwa ubunifu wao wa kujenga majengo hayo sehemu mbalimbali nchini pia amesisitiza majengo hayo yajengwe karibia nchi nzima ikiwezekana watafute soko la ujenzi nchi za nje.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba nchini, Maulid Banyani, amesema katika mwaka huu wa fedha shirika hilo linatarajia kujenga majengo kama hayo katika Mkoa wa Lindi na Kagera.

Majaliwa hakuishia hapo pia amezindua soko la pamba katika chama Cha msingi cha ushirika katika Kata ya Kasekese Mkoani Katavi na kusema kuwa mwaka huu soko la pamba limeshuka kutokana na ugonjwa wa Corona.

Aidha, amesema wanunuzi wengi wa pamba ni kutoka nchi za nje hivyo corona imewazuia kuja kununua pamba nakufanya soko la pamba kushuka kuto shilingi 1,200 kwa kilo hadi shilingi 810.

Kwa upande wao wakulima wa zao la pamba Mkoani humo wameiomba serikali kuwapa elimu ya utumiaji wa mizani ya kupimia pamba hizo ilinawao waweze kujua namna ya upimaji kuepuka kuibiwa pointi zinazozidi katika kilo.

Habari Kubwa