Mwana FA asimulia alivyonusurika kifo kwenye ajali

31Aug 2021
Idda Mushi
MOROGORO
Nipashe
Mwana FA asimulia alivyonusurika kifo kwenye ajali

Watu watano pamoja na Mbunge wa Jimbo la  Muheza Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wamenusurika kifo katika ajali baada ya magari waliyokuwa wakisaifiria kugongana katika eneo la Mkambalani, Barabara Kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro jana usiku baada ya kutokea ajali hiyo, amedai alikuwa  kwenye gari na dereva wake, na wote wamenusurika isipokuwa yeye amepata maumivu kidogo maeneo ya kifuani na dereva wake ambaye amepata michubuko kidogo.

Akizungumza Kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim amekiri kutokea Kwa ajali hiyo nachazo ni gari ndogo aina ya Crown kujaribu kulipita gari jingine na kugongana na gari iliyokuwa imembeba Mbunge huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shighela aliyefika hospitalini hapo na Mkuu wa Wilaya Albert Msando, amevitla Vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza chanzo cha ajali na madereva na watumiaji wengine wa Barabara kuchukua Tahadhari hasa ikizingatiwa Morogoro imekuwa ikipitisha magari mengi kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.