Mwana FA apata kigugumizi kisa ushindi

01Nov 2020
Steven William
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Mwana FA apata kigugumizi kisa ushindi

MBUNGE  Mteule wa  Muheza. Hamisi Mwinjuma, maarufu kama Mwana FA, ameshikwa na kigugumizi na kushindwa kuzungumza mbele ya waandishi wa habari kutokana na furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, Nasibu Mbaga, alimtangaza Mwana FA kuwa ndiye mshindi wa ubunge kwa kupata kura 47,578 na kumwacha mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyepata kura 12,036.

Mwana FA alishindwa kujieleza kwa muda mrefu kutokana na furaha ya ushindi mnono aliyoupata.

“Jamani sijui niseme nini maana nina furaha kubwa sana kwa ushindi niliopata.  Nawashukuru sana wananchi wa Muheza kwa kunichagua kuwa mbunge wenu. Tutashirikiana katika kuleta mendeleo ya Muheza,” alisema baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi.......kwa taarifa zaidi fuatilia epaper.ippmedia.com

 

Habari Kubwa