Mwanaharakati ataka wanafunzi wasijiue, kisa matokeo

12Oct 2019
Zanura Mollel
Longido
Nipashe
Mwanaharakati ataka wanafunzi wasijiue, kisa matokeo

MWANAHARAKATI wa kupinga na kupambana na ukeketaji kwa watoto wa kike wilayani Longido kutoka shirika la TEMBO TRUST ,Mery Laizer (Tembo) amewataka wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Longido kuepuka tabia ya kujinyonga pindi matokeo yanapokuja tofauti na alivyofikiria.

Mery Laizer akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Wa kidato cha nne, ambaye pia ni mwanajumuiya ya UKWATA shule ya sekondari Longido

Akizungumza kwenye mahafali ya dini (UKWATA) iliyofanyika Leo shuleni hapo, Laizer ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, amekemea vikali maamuzi ya baadhi ya wanafunzi kukata tamaa matokeo yanapokuja tofauti, na kuwataka kutambua kua kuna maisha baada ya elimu.

Katika mahafali hayo ,amekabidhi Spika yenye mdundo yenye thamani ya Tsh 900,000 vitambaa vya ibada Tsh 180,000, microphone Tsh 150,000 na fedha taslimu sh 800,000 ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto walizonazo wanajumuiya ya UKWATA.

Baadhi ya Wanafunzi na wanajumuiya UKWATA , wa shule ya sekondari Longido wakifurahia Zawadi ya Speaker.

Habari Kubwa