Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

05May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Halima Cisse, mwenye umri wa miaka 25, amejifungua watoto tisa, kati yao wa kike watano na wavulana wanne.

Cisse, alijifungua katika hospitali iliyopo ya Morocco Jumanne ambako alikuwa amelazwa.

Waziri wa Mali, Fanta Siby alitoa taarifa hiyo na kwamba mama huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji.

Cisse alikuwa akitarajia kijifungua watoto saba, kutokana na uchunguzi wa picha ya skani tumboni ilivyoonyesha.

Uchunguzi huo alifanyiwa nchini Mali na Morocco ingawa haikugundulika amebeba watoto wengine wawili.

Jumanne, Dk. Siby alisema watoto hao na mama yao wanaendelea vyema na wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, akisema ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu.

Mimba Cisse, ilishangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na iliwavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo, huku baadhi yao wakisafiri hadi Morocco kwa mazungumzo ya kitaalamu, shirika la habari la Reuters, liliripoti.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Morocco, Rachid Koudhari, aliliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.

BBC

Habari Kubwa