Mwanamke akamatwa kwa kuishi na wanaume wawili nyumba moja

25Sep 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mwanamke akamatwa kwa kuishi na wanaume wawili nyumba moja

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Maurine Atieno mkazi wa kijiji cha Chamgiwadu kaunti ya Migori, amekamatwa na polisi nchini Kenya pamoja na wanaume zake wawili aliokuwa akiishi nao.

picha hii ya mitandao haihusiani na habari.

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya majirani kulalamika na kutaka mamlaka husika kumchukulia hatua wakidai kitendo hiko sio sahihi.

Chifu wa eneo hilo David Onyango amesema kwamba mwanamke huyo amekuwa akiishi na waume hao wawili kwa pamoja kama waume zake wa ndoa, kwa muda wa wiki mbili sasa ndani ya nyumba moja.

Ndoa hiyo ya mitala kwa wanaume hao ilitokea pale baada ya Maurine ambaye aliolewa na Robert Ochieng ambaye pia amezaaa naye watoto wawili, kurudi nyumbani akiwa na mpenzi mpya aliyetambulika kwa jina la John Ochola aliyempata kwenye shughuli zake za kuuza samaki huku akimtaja kuwa mteja wake muaminifu, na kuamua kuishi nao wote kwa pamoja.

Chifu huyo ameendelea kwa kusema kwamba wanachunguza ni kwa namna gani watatu hao wamekubaliana kuishi ndani ya nyumba moja, na kwamba ndoa hiyo ya pili ya Maurine na John imethibitishwa na mama wa John ambaye amekiri na kusema kwamba mkwe wao huyo huwa anaenda mara kwa mara kuwatembelea nyumbani kwao.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umesema kwamba hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kuwashtaki, isipokuwa wataangalia namna ya kuwatenganisha watatu hao, ili kuepusha majanga yoyote ambayo yanaweza tokea.

Habari Kubwa