Mwangosi akumbukwa kwa kuhimiza uhuru wa habari

03Sep 2017
Rose Jacob
Nipashe Jumapili
Mwangosi akumbukwa kwa kuhimiza uhuru wa habari

WATANZANIA wamehimizwa wasikae kimya bali wawe mstari wa mbele kupinga njama za kuminya uhuru wa tasnia ya habari kwa vile unaathiri kila mmoja.

tukio lililosababisha askari polisi kumpiga risasi ya tumbo daudi Mwangosi na kufariki hapohapo.

Wameambiwa kuwa kuunyamazisha uhuru wa kujua si kwamba kunawaumiza wanahabari au wamiliki wa vyombo vya habari pekee, bali hata umma ambao unastahili kujua na kuelewa mambo yanayolihusu taifa na maslahi yao, unakandamizwa pia.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habarai Tanzania, Abubakar Karsan, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, aliyeuwawa na polisi Septemba 2,2012 wakati akiwa kazini katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.

“Watanzania wafahamu serikali inayominya uhuru wa habari haiwanyimi haki waandishi wa habari tu,bali watambue na wao wana jamii hawatakuwa na uhuru wa kuzipata habari zinazostahili hususani katika kukosoa yanayofanywa na serikali, inaonyesha wazi kutokutambua umuhimu wa habari katika ujenzi wa taifa,”alisema Karsan.

Aidha,aliwaomba Watanzania kushikamana na waandishi katika kulinda maslahi ya kazi yao kwa kuwawezesha,maana mazingira wanayofanyia kazi ni magumu hususani katika mishahara.

Alisema UTPC haikubaliani na kipengele cha sheria mpya ya habari ya mwaka 2016,kinachowataka waandishi wa habari wawe na Diploma na kuendelea kusajiliwa na kutoa vitambulisho kwa waandishi ili wafanye kazi jambo ambalo si sahihi linalominya demokrasia na upatikanaji wa habari.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Osoro Nyawanga, aliwataka wanahabari na wadau kuacha kubweteka kwa kigezo cha habari ni muhimili wa nne wa serikali, jambo ambalo lina wagharimu kutokana na kukosa ajenda inayoweza kuisaidia tasinia hii, ili serikali ione ni wapi ilipokosea na iache kuidhalilisha tasnia hii.

Habari Kubwa