Mwanri: Magufuli 'Katushka' ya Tanzania iliyoondoka duniani

21Mar 2021
Godfrey Mushi
SIHA
Nipashe Jumapili
Mwanri: Magufuli 'Katushka' ya Tanzania iliyoondoka duniani

MKUU wa mkoa mstaafu wa Tabora, Aggrey Mwanri amemfananisha hayati Rais Dk. John Magufuli na silaha ya kivita ya Urusi aina ya 'Katushka', iliyoondoka duniani, licha ya kuaminiwa sana.

Magufuli alifariki dunia, Machi 17mwaka huu katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Leo, akizungumzia uzalendo na uwezo aliokuwa nao wa kulisaidia taifa hayati Rais Magufuli, Mwanri amesema;

“Ile silaha inaitwa katushka nilenda kuiangalia, nilikuwa sujui maana yake. Ikishapigwa ile na Warusi wakiona imeshindwa kutumika, wanasema sasa kila mtu akimbilie.

“Ni maoni yangu, kwa mtu ambaye nilipata heshima ya kufanya kazi na kiongozi huyu (Magufuli), kilichoondoka duniani ni katushka."

 

Habari Kubwa