Mwenyekiti mpya AU aapa kupambana na ugaidi

11Feb 2019
Salome Kitomari
Addis Ababa,Ethiopia
Nipashe
Mwenyekiti mpya AU aapa kupambana na ugaidi

Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Nchi za Afrika, ambaye ni Rais wa Misri, Fatal Al Sisi, amesema kwa kipindi cha uongozi wake atahakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarika barani Afrika,ikiwamo kuwasaka wanaowafadhili magaidi.

Rais wa Misri, Fatal Al Sisi.

Ameyasema hayo wakati akihutubia wakuu wa nchi za Afrika kwenye mkutano wa 32 unaoendelea mjini Addis Ababa,Ethiopia,uliowaleta pamoja marais na wawakilishi wao wa nchi 48 za Afrika.

Amesema anajua jinsi ilivyo ngumu kukabili suala la ugaidi lakini kwa umoja Afrika inapaswa kuwajua wanaowafadhili na kuchukua hatua.

Amesema ugaidi umeghariku maisha ya watu na kukatisha ndoto zao ikiwa ni pamoja na kuharibu uchumi wa nchi husika,na kwamba Kenya imekuwa mhanga wa matukio hayo mara kwa mara.

Katika mkutano huo Tanzania imewakilishwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,ambaye amembatana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Augustine Mahiga.

Habari Kubwa