Mwijage apigia debe viwanda vidogo

25Apr 2018
WAANDISHI WETU
MLANDIZI
Nipashe
Mwijage apigia debe viwanda vidogo

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage, amesema ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati una tija kuliko viwanda vikubwa.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage

Alisema viwanda kidogo na vya kati vina urahisi kwenye uendeshaji na uzalishaji wake ni wa haraka unaochochea maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla

Mwijage aliyasema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi kati- ka ujenzi wa kiwanda cha Kemikali cha Msufini kinachojengwa katika kijiji cha Msufini, Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani.

Mwajage alimwakilisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kati- ka uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo wa ubia kati ya kampuni ya Junaco ya nchini na Serba ya nchini Malaysia.

“Viwanda kama hiki vikubwa ni vizuri lakini viwanda vyenye tija na vinavyoweza kuajiri watu wengi ni viwanda vidogo ambavyo vinaweza kusambaa maeneo mengi nchini,” alisema Mwijage.

Alisema viwanda vidogo na vya kati vinajenga uchumi jumuishi na kuajiri watu wengi na kusambaa maeneo mbalimbali tofauti na vikubwa.

“Itakuchukua muda watu kue- lewa, ikipendeza Mheshimiwa Rais John Magufuli azidi kuniweka hapa hadi 2025 ili nikamilishe kazi hii,” alisema Mwijage.

Naye Mtendaji Mkuu wa Junaco, Justine Lambert, alisema ujenzi wa mradi huo utagharimu Sh. bilioni 256.

Alisema kiwanda hicho kikubwa na cha kwanza kuwapo nchini, asil- imia 80 ya dawa zitakazozalishwa zitauzwa nje ya nchi zikiwamo za Afrika na Ulaya na asilimia 20 zitauzwa nchini.

Alisema kiwanda hicho kitajengwa eneo lenye ukubwa wa heka nane, kitakamilika kwa miaka miwili na baada ya kukamilika kitatoa ajira rasmi 700 kwa vijana wa Kitanzania.

“Kiwanda hiki kitajengwa ndani ya miezi 23 na kitatoa ajira za muda mrefu na muda mfupi kwa wazawa lakini pia ajira rasmi kwa vijana 700 baada ya kukamilika,” alisema Lambati.

Aidha, alisema kwa kipindi cha miaka 10 wataalam kutoka nje ya nchi watawapatia mafunzo wa- handisi wa ndani ya nchi namna ya kuendesha ili kuwa na wataalam wa kutosha nchini.

Alifafanua zaidi kuwa, mfumo wa uzalishaji wa kemikali huo utahitaji chumvi, maji na umeme na kemi- kali hizo zitatumia kusafisha maji na katika viwanda kikiwamo cha mabati. 

“Bidhaa hii imekuwa ikiagizwa nje ya nchi lakini sasa itapati- kana nchini kwa gharama nafuu, lakini pia itasaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa gharama nafuu zaidi endapo mamlaka husika zitatumia

dawa hizo na kufikia lengo la serikali la upatikanaji maji safi na salama maeneo yote nchini kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2020,” alisema.

Alisema faida nyingine ni kuliingizia taifa fedha za kigeni, kukuza uchumi na kuongeza kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa taifa.

Lambert alisema kwa wingi wa bidhaa zitakozalishwa katika kiwanda hicho watalazimika kuagiza chumvi kutoka nje ya nchi hadi hapo soko la ndani litakapokidhi mahitaji.

Pia alitaka serikali kulinda bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi ili bidhaa zinazotoka nje ya nchi zisiingie nchini na kuharibu soko.

Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi, aliahidi kuzindua kiwanda kingine wilayani Baga- moyo mkoani humo kutokana na eneo hilo kuwa kivutio cha amani na utulivu.

Dk. Mengi alisema mkoa huo una mtaji mkubwa wa amani ambayo inavutia wawekezaji kufanya hivyo na kuwasihi kue- ndelea kuitunza.

“Niwapongeze watu wa Pwani kwa kuwa watulivu na amani, hongereni sana. Amani ni rasilimali kubwa kuliko vingine vyote, ni muhimu kuliko fedha, magari na viwanda hivyo nawasihi muendelee kuitunza,” alisema Dk. Mengi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema kiwanda hicho kitapokea tani 2,500 za chumvi isiyo na madini joto kila mwezi kwa ajili ya uzalishaji.

Alisema vijana wa mkoa huo wameajiriwa kwa asilimia 20 katika viwanda vilivyopo mkoa- ni huko na kwamba kuendelea kufunguliwa kwa viwanda ajira zinaongezeka. 

Habari Kubwa