Mwili waokotwa kwenye kiroba Dar es salaam

16Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mwili waokotwa kwenye kiroba Dar es salaam

Mwili wa mtu mmoja umeokotwa eneo la sayansi jirani na Chuo cha Ustawi wa jamii ukiwa umefungwa kwenye kiroba.

Askari polisi wakipakia mwili wa mtu huyo kwenye gari la polisi.

ITV imefika katika eneo hilo na kushuhudia kiroba hicho ambacho baadae kilichunguzwa na maafisa usalama na kugundua ni mwili wa binadamu.

Mjumbe wa mtaa huo Bi Fortunata Mshindo akizungumza na ITV amesema mchana yeye na wananchi wengine walipita katika eneo hilo na hakukua na kitu chochote huku pia akisisitizia uongozi wa manispaa kuweka taa katika eneo hilo ili kupunguza matukio ya kihalifu.

Chanzo ITV