Mwinyi aeleza sababu ya kuwa na amani nchini

20Nov 2019
Ibrahim Joseph
DODOMA
Nipashe
Mwinyi aeleza sababu ya kuwa na amani nchini

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk,Husein Mwinyi  amesema Amani iliyopo Nchi haitokani na ukubwa wa majeshi au  uwingi wa Askari ila inatokana na utulivu wa Wananchi.

Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa sherehe za maulidi zilizofanyika kwenye msikiti wa Dodoma Sunni Nunge uliopo Jijini hapa.

Dk, Mwinyi alisema amani iliyopo nchini haitokani na ukubwa wa majeshi au uwingi wa askari ila inatokana na utulivu wa wananchi wote kuendelea kuilinda.

“Wapo watu wanaodhani kuwa ukiwa  na majeshi makubwa au ukiwa polisi wengi ndipo  utakapopata amani ,sivyo,vyombo vya ulinzi na usalama havileti amani wanaoleta amani ni wananchi ”alisema.

Alisema yapo mataifa ambayo yalikuwa na amani na majeshi mengi lakini walipoichezea amani wameingia kwenye vita na machafuko ambayo hayajulikani mwisho wake utakuwa lini.

Alisema Mataifa hayo yalikuwa na askari na majeshi mengi lakini amani ilipotoweka wameshindwa kuirudisha na kuzalisha uchumi kila siku ni machafuko watu hawana uhakika wa kuiona kesho yao.

Aliyataja baadhi ya mataifa yaliyoingia kwenye machafuko baada ya wananchi wake kuiondoa amani na sasa hawana amani kuwa ni Libya,Siria,Algeria,Siera leoni,Congo DRC,Yemen na mataifa ya Sudan.

“Sasa sisi mwenyezi Mungu ametujalia amani ndani ya nchi yetu, kwa hivyo tujitahidi kuilinda amani yetu, ili kuweze kufanya mambo yetu ya kimaendeleo lakini na kufanya ibada kwa utulivu kama hivi”alisema.

Habari Kubwa