Mzozo wa vyeti  wahitimu, chuo

06Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mzozo wa vyeti  wahitimu, chuo

Zaidi ya wahitimu 100 wa kozi ya Afya ya Jamii katika Chuo cha Sayansi ya Afya cha St. Agrey  jijini Mbeya, wanakusudia kukifungulia mashtaka chuo hicho kwa madai ya kupoteza vyeti vyao vya kidato cha nne.

Rais mstaafu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Noel Mng’ong’o, anasema wakati wanajiunga na chuo hicho Novemba 2015, waliambiwa wapeleke vyeti vyao halisi  ili vipelekwe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya uhakiki.

Anasema vilikusanywa vyeti vya wanafunzi wa kozi zote na vingine vilirejeshwa baada ya uhakiki isipokuwa vya wanafunzi wa kozi ya afya ya jamii ambayo tangu wakati huo wamekuwa wakifuatilia bila mafanikio.

Mng’ong’o anasema awali walikuwa na matumaini kuwa vyeti vyao vingepatikana, lakini matumaini hayo yalianza kufifia wakati wanakaribia kumaliza masomo kwa madai kuna mmoja wa watumishi wa chuo hicho aliwadokeza kuwa vyeti vyao havijulikani vilipo.

Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Rex Mwakipiti, anakiri kukusanya vyeti vya wanafunzi hao, lakini alisema ni vyeti vya wanafunzi  102 na siyo 111 kama inavyodaiwa.

Habari Kubwa