Nashukuru ila Sinafuraha - Aida Khenani Mbunge Pekee Chadema

31Oct 2020
CHADEMA BAADA YA UCHAGUZI 2020
Nipashe
Nashukuru ila Sinafuraha - Aida Khenani Mbunge Pekee Chadema
  • “Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu, nitungana na wenzangu nakufwata maamuzi yoyote ya chama changu”

Baada ya kutangazwa mshindi jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenani wa Chadema anamshukuru Mola kwa ushindi huo ila ‘ushindi wenye sio wa furaha’ asema.

Mheshimiwa Aida Khenani, mshindi wa pekee kiti cha ubunge Chadema. (Picha na Dar24)

Baada ya kutangazwa mshindi jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenani wa Chadema anamshukuru Mola kwa ushindi huo ila ‘ushindi wenye sio wa furaha’ asema.

Akiweka maoni yake wazi kupitia mtandao wa Twitter, Mheshimiwa Khenani amesema demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wake na yupo tayari kufwata maelekezo ya chama chake.

Mbunge huyo amejikuta yuKo peke yake kwenye jukwa la ushindi la chama chake cha Chadema baada ya wogombea wenzake wakiwemo viongozi wa chama hicho kupigwa chini katika nafasi walizo gombea.

Hii inamaana kuwa, Mheshimiwa Khenani atakuwa mbunge pekee wa Chadema ‘mjengoni’ bunge litakapo anza kazi zake tena.

Khenani alibuka mshindi baada ya kupata kura 21,226 na kumshinda Ally Keissy wa CCM aliyepata kura 19,972.

Hayuko peke yake, chama cha upinzani cha CUF nacho kimekumbwa na janga hilo hilo baada ya kupata kiti kimoja tu bungeni.

Kwenye jimbo la Mtwara Vijijini, Shamsia Mtamba ameshinda kiti cha ubunge baada yakupata kura 26,262, na kumshinda mbunge mtetezi wa jimbo hilo kupitia CCM Hawa Ghasia aliyepata kura 18,505.

Kwa uchambuzi wa kina wa Uchaguzi 2020 bofya hapa: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa