Nchi 7, ikiwemo Tanzania kuekewa vikwazo kuingia Marekani

22Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Nchi 7, ikiwemo Tanzania kuekewa vikwazo kuingia Marekani

TANZANIA imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi saba ambazo raia wake watakumbana na vikwazo pindi watakapohitaji kuelekea nchini Marekani.

Rais wa Marekani, Donard Trump

Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari leo, Kaimu Balozi wa Marekani, Dkt Inmi Patterson, amethibitisha kauli hiyo mara baada ya taarifa hizo kuanza kusambaa katika mitandao ya kijamii, huku nchi nyingine zikitajwa kuwa ni pamoja na Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria na Sudan.

Hata hivyo, gazeti la Wall Street limefanya mahojiano na  Rais wa Marekani, Donard Trump ambaye kwa sasa yupo kwenye kongamano la uchumi linaloendelea huko Dacos nchini Switzerland kuhusiana na suala hilo lakini hakutaja nchi hizo na kusema kuwa taarifa rasmi itatoka mwezi ujao.

Taarifa ya mtandao wa Politico imeeleza kuwa nchi hizo zinaweza kufahamika Januari 27, Mwaka huu.

Habari Kubwa