Ndege ya Ethiopia yatua Mwanza yabeba minofu samaki kwenda Ubelgiji

22May 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Ndege ya Ethiopia yatua Mwanza yabeba minofu samaki kwenda Ubelgiji

Ndege ya Ethiopia  Boeing 787-8 aina ya Dream Liner yenye usajili ET-ARE kwa mara ya kwanza yatua nchini kubeba minofu ya samaki na mabondo kwenda Brussels nchini Ubelgiji hiyo ikiwa ni mara ya tatu kwa minofu ya samaki kutoka nchuni kusafirishwa  kuelekea nchini humo.

Ndege ya Ethiopia ikiwa tayari kubeba minofu ya samaki.

Mzigo uliosafirisha ni zaidi ya tani 19 zilizotumia USD 79820 gharama za usafirishaji na kwamba Kampuni ya Victoria Perch Limited ambao wamesafirisha tani 5.4 kwa USD 21,600, Nile Perch Limited  tani 8.9 kwa USD 35,900 na Omega Fish Limited tani 5 kwa USD 22,320.

Akizungumza wakati akishuhudia ndege hiyo ikipakia mizigo hiyo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amewataka wananchi kufanya kazi hasa uvuvi wa kisasa kwa sababu soko lipo hivyo ni wakati wa kufanyakazi usiku na mchana ili kuleta maendeleo na kuongeza chachu ya ushindani katika usafirishaji mzigo kwenda Ulaya.

Amesema kazi itaendelea kufanyika kama ilivyopangwa na wiki ijayo ndege hiyo itarejea nchini na kubeba tani 40  huku akiwaomba Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli  kwa sababu amefanya vitu vya kipekee ili na yanayotendeka ni maono yake.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, amesema mapambano ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na kirusi aina ya COVID-19 yanaendelea huku juhudi za kukuza uchumi wa nchi zikipamba moto anaeleza Tanzani kuna samaki wazuri na wakutosha na soko la uhakika lipo hivyo wawekezaji watumie fursa hiyo kwa kuwaTanzania ni mahali sahihi pakuwekeza.

Ameongeza kuwa ujio wa ndege hiyo umeongeza ajira, dunia kufahamu utamu wa samaki wa Tanzania,kujenga mahusiano mazuri  sambamba na kutambua ni mahali pazuri na salama kuwekeza na kufanyabiashara pia aliwataka wananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya ili kujilinda na ugonjwa huo ili shughuli za uzalishaji ziendelee.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema ndege hiyo ya Ethiopia ni mara ya kwanza kubeba minofu hiyo ndani ya mkoa huo ambapo mashirika mengine yanatarajia kuja,nguvu na maono aliyoyaweka Rais kuliinua taifa na kuwaletea maendeleo wananchi yametimia hivyo utekelezaji wa kazi utaleta tija na thamani katika maisha ya wananchi na kuongeza uchumi wa kanda ya ziwa.

Amesema kuwa wavuvi wataendelea kupiga kazi ipasavyo ili kunifaika na kuona thamani ya samaki kwani biashara imeanza kupanda hivyo wafanye kazi ili kuendana na  fursa hiyo .

Meneja Ubora kutoka Victoria Perch Limited, Dk. Edwin Okong’o ametoa shukrani kwa serikali kwa kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa sasa watasafirisha moja kwa moja  na kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata mwanzo pia opration sangara imesaidia kuzalisha  samani wengi na wenye viwango ndani ya ziwa Victoria na kuwapa uhakika wa upatikanaji wa samaki na soko kuwa la uhakika.

“Leo tunasafirisha mzigo tani 5.4 wenye thamani ya USD 21,600  mwanzo tulikuwa tunasafirisha kupitia Uganda ama Kenya tulikuwa tunapata usumbufu mkubwa barabarani sisi tumeshakubwa na adha mbalimbali ikiwemo ya kupoteza mzigo ,kuvamia na kupolwa ,gari kuanguka na wakati mwingine kukosa ndege baada ya kufika nje ya muda sasa mzigo unaenda kwa wakati na samaki wanakuwa freshi na kuongeza uthamani wake” amesema Okong’o.

Aidha Meneja wa Nile Perch Fisheries Limited Ruesh Mohan, amesema ni mara yao ya pili kusafirisha minofu ya samaki kutoka nchini kwenda Ubelgiji ambapo kwa wakati huu wamesafirisha tani 8.9 yenye thamani ya USD 35,900  hivyo alitoa shukrani kwa Rais na timu yake kwa kufanikisha kuwaletea ndege katika uwanja wa Mwanza wataitumia fursa hiyo ipasavyo.

“Corona ikipungua ama kuisha soko litafunguka zaidi na biashara kuongezeka kwani hali ilivyosasa kwa wiki tunapeleka tani 80  lakini ikiwa vizuri tunaweza kupeleka tani 200 kwa wiki pia kwa sasa samaki wamepungua kutokana na hali ya hewa”amesema Mohan.

Habari Kubwa