Ndoa hiyo ya kijeshi ilifungwa mwisho ni mwa wiki jijini Arusha na kuudhuriwa na viongozi waandamizi wa jeshi hilo na viongozi wa serikali.
"Kwa kweli imekuwa siku muhimu katika maisha yangu kwa kufanya jambo la kipekee ambalo linafungua njia na taswira nyingine kwa sisi wawili,"alisema Sumai.
Alisema kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine Mungu amependa wawili hao kuwa kitu kimoja na kwenda kuanzisha mchakato wa maisha mapya ambayo yatakuwa sehemu kuunda familia bora na imara itakayokuwa ya mfano katika Jamii.
"Tuna mshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli yetu ya ndoa hii kufungwa nina furaha na tunatarajia kuishi maisha ya furaha na upendo ambayo yatakuwa mfano kwa wengine kuiga,"aliongeza.