Ndugai amuonya Nape kuhusu wabunge Chadema

03May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ndugai amuonya Nape kuhusu wabunge Chadema

SPIKA wa bunge ,Job Ndugai amemuonya mbunge wa Mtama Nape Nnauye kwa kile alichokiita kuwasema vibaya wabunge wenzake ambao ni wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema kitendo hicho hakina tija kwa bunge hilo.

Akizungumza bungeni  leo ,Spika Ndugai amesema kuwa kwa mujibu wa Kanuni za bunge hilo ni kosa kuwasema vibaya wabunge wengine.

“Majuzi imetokea maneno kidogo ,mdogo wangu Nape yakamtoka maneno kidogo na yamezunguka sana ,sasa kwa sababu ni mbunge ikifika mahali mbunge na Spika muwe mnapishana nadhani haipendezi “-amesema Spika Ndugai.

“Sitapitia hoja zake kwa sababu ana uhuru hata hivyo, lakini kitu kimoja hana uhuru kwa sababu ya kanuni ni kuwasema vibaya wabunge wenzake kwa majina hilo lazima nilikemee”-amesema

Wabunge hao 19 wa Viti Maalum ambao aliwasema Nape wakati akichangia mawazo yake katika mdahalo uliofanyika kwa njia ya mtandao ukiwahusisha viongozi wengine wa Vyama vya Siasa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo ni pamoja na Halima Mdee, Ester Matiko, Ester Bulaya na Nusrat Hanje.

Wengine ni Grace Tendega, Cecilia Pareso, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Felister  Njau, Kunti  Majala, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza, Anatropia Theonest  ,Naghenjwa Kaboyoka na Agnester  Lambart.

Habari Kubwa