Ndugai atangaza jimbo la Buhigwe kuwa wazi

30Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Ndugai atangaza jimbo la Buhigwe kuwa wazi

SPIKA wa bunge Job Ndugai amelitangaza rasmi jimbo la Buhigwe alilotoka Dk.Philip Mpango kuwa wazi ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo kuthibitishwa rami na bunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kura zilizopigwa bungeni na matokeo yake kutangazwa na Spika Ndugai wabunge wote 363 waliokuwemo bungeni sawa na asilimia 100 wamemthibitisha Dk.Mpango kuwa Makamu wa Rais jambo lililopelekea jimbo lake kuwa wazi.

Nafasi ya Makamu wa Rais imekuwa wazi tangu kuapishwa kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Dkt.John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.

Dkt.Magufuli aliyefariki kutoka na tatizo la umeme wa moyo alizikwa katika makazi yake yaliyopo Chato Mkoani Geita Machi 26 mwaka huu huku viongozi mbalimbali wa kitaifa wakihudhuria mazishi yake.

Habari Kubwa