Ndugai awataka mawaziri, Wabunge kuhudhuria bungeni kesho

21Apr 2021
Gwamaka Alipipi
Dodoma
Nipashe
Ndugai awataka mawaziri, Wabunge kuhudhuria bungeni kesho

SPIKA Job Ndugai, amewataka mawaziri na wabunge wote waliopo nje ya Jiji la Dodoma kuacha shughuli wanazofanya na kurejea haraka Dodoma, kuhakikisha kesho wanakuwapo bungeni kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan.

SPIKA Job Ndugai.

Amesema hotuba itakayotolewa kesho na Rais Samia ni muhimu kwa wabunge wote na Watanzania, hivyo ni lazima kila waziri, mbunge kuwamo bungeni.

Kwenye taarifa yake Spika Ndugai alisema: "Naomba nisisitize kwamba kesho kila mtu lazima awepo bungeni. Naomba wabunge muwaambie wenzenu ambao hawapo Dodoma. Hata mawaziri waache shughuli zao warejee bungeni. Itakuwa jambo la aibu wageni kujaa kila sehemu ya bunge alafu ndani ya Bunge kuna ma-gap ( nafasi) wabunge hawapo".

Habari Kubwa