Ndugai azionya Azaki kuacha kutumika

23Oct 2021
Marco Maduhu
Dodoma
Nipashe
Ndugai azionya Azaki kuacha kutumika

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amezionya Asasi za kiraia hapa nchini kuacha kutumika vibaya.

Spika Job Ndugai akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa asasi za kiraia.

Ndugai amebainisha hayo leo, wakati akifungua wiki ya asasi za kiraia hapa nchini, katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Amesema baadhi ya asasi za kiraia, zimekuwa zikitumika vibaya kuichafua nchi, na kujifanya wao kila siku ni wakosoaji.

"Ujumbe wangu wa leo kwa asasi za kiraia acheni kutumika, na ndiyo maana zinatungwa sheria za kuwabana, sababu ya mienendo yenu, bali kuweni wazalendo, na kuipenda nchi yenu," amesema Ndugai.

Aidha, amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa asasi za kiraia hapa nchini, katika kuwa hudumia wananchi, ambapo wamekuwa wakifika kwenye maeneo ambayo Serikali haiwezi kufika na kusaidia makundi mbalimbali,

Pia, amezitaka Asasi za kiraia ziendelee kuomba fedha ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yao kwa maendeleo ya taifa.

Katika hatua nyingine Spika Ndugai, ameahidi Ofisi ya Bunge kuendelea kushirikiana na asasi za kiraia hapa nchini, kwa mstakabali wa maendeleo ya Taifa.

Habari Kubwa